CROWN FM: Radio Mpya ya Alikiba

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya na mjasiriamali, Alikiba, ameandika historia mpya katika tasnia ya burudani nchini Tanzania kwa kuzindua kituo chake kipya cha redio kinachoitwa CROWN FM.

Alikiba azindua Radio Mpya inaitwa CROWN FM

Alikiba azindua Radio Mpya inaitwa CROWN FM

Alikiba ameeleza sababu za kuzindua Radio kuwa ni njia pekee iliyoinua career yake na watu kumfahamu kupitia Radio.

Baada ya kuwa msanii kwa takribani miaka 20 sasa anakuwa miongoni mwa Wasanii na watu wanaomiliki Radio.

Sababu ya Alikiba kuanzisha media

Kwa miaka ishirini iliyopita, Alikiba amekuwa ikoni katika muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania na kimataifa. Kupitia kazi zake zenye nguvu, ameifanya Tanzania kuwa kitovu cha muziki wa Kiafrika na kuhamasisha vijana wengi katika tasnia ya burudani.

Uzinduzi wa CROWN FM unawakilisha mwanzo mpya katika safari ya Alikiba kama mjasiriamali wa muziki na utangazaji. Kituo hiki kinatoa fursa kwa wasanii wapya na wanaokua kutangaza muziki wao, na pia kuwapa mashabiki upatikanaji wa moja kwa moja wa burudani bora. Kupitia CROWN FM, Alikiba anajenga jukwaa la kipekee la kuelimisha, kuburudisha, na kukuza vipaji vipya katika tasnia ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *